SIR RATCLIFFE


 

Mmiliki mwenza mpya wa Manchester United, Sir Ratcliffe ambaye anamiliki asilimia 27.7 za hisa za klabu hiyo ameelezea msimamo wa Mashetani hao Wekundu kuhusu mshambuliaji Mason Greenwood ambaye anakipiga kwa mkopo Getafe.


MASON GREENWOOD



"Ni uamuzi mpya kwa upande wetu, yeye ni mchezaji wa Man United na tutaanza mchakato wa kuamua juu ya mustakabali wake" amesema Ratcliffe 


"Tunahitaji kuangalia ukweli, kuhukumu kwa haki na kuzingatia maadili ya Man United yanasemaje. Tutajaribu kuelewa ukweli na sio kukurupuka”


"Tutatumia maadili kama ni mtu mzuri au la, kama ataweza kucheza kwa dhati kwa ubora, na ikiwa tutafurahia uwepo wake, mashabiki wataridhika naye.. basi tutaona".

Manchester United Swahili.


Comments

Popular posts from this blog

U18

CV ZA WACHEZAJI WA MAN U 2023/2024

MECHI ZA MWEZI WA 2/3